6.1 Ukweli kuhusu Mfumo wa Hukumu
6.1 Facts about the Ruling System
Mfumo wa Utawala wa Kiislamu umejengwa juu ya mfumo wa kipekee wa umoja ulioamriwa na Allah (SWT). Si mfumo wa kishirikisho, wa kidemokrasia, wa kijamhuri, wa kifalme wala wa kidikteta hata kidogo. Hauna mfanano wowote na itikadi yoyote iliyobuniwa na binadamu.
The Islamic Ruling System is based upon a unique system of unity ordained by Allah (swt). It is not a federal, democratic, republican, monarchical or dictatorial system at all. It has no similarity to any man-made ideology.
Dola ya Kiislamu inawachukulia watu walio chini ya mamlaka yake kuwa raia, iwe ni Waislamu au wasio Waislamu. Wote wana haki zao zilizohakikishwa na Uislamu. Hakuna dhana ya 'wachache wa kikabila' kwa kuwa watu hawabaguliwi hata kidogo kwa sababu ya rangi yao, kabila lao au dini yao.
The Islamic State considers people under its authority as citizens, whether they are Muslims or non-Muslims. All have their rights guaranteed by Islam. There is no concept of ‘ethnic minority’ as people are not discriminated against at all due to their colour, race or religion.